Usanii wa Sanaa

Jo ni msanii flani,
ana tamaa ya kuboresha hii fani,
na kusambaza upendo kwa mashabiki kwote mitaaani,
lakini bila pesa,
hana chakuotesha,
mavuno yake ya siku za  usoni ni kama ndoto,
kila kukicha njiani yu kaguu,
akisaka producer wa bei nafuu,
nyumbani wazazi wamuona kapotoka na kuiga tabia za kigeni,
pia nyimbo zake ni za ushenzi,
mabeste nao Jo kwao ni kikwazo,
leo hiii ameketi kazingirwa na mawazo,
kujiuliza nivipi nitapenya,
na mziki wangu kupendeza,
bila heshima kupoteza,
Mungu wangu nilitendani,
ndio napata shida kama hizi,
sina tamaa ya kujulikana,
bali nina mori wa kuonyesha vijana,
kuwa dunia ni duara hakuna pa kujificha,
lazima ukweli utakuumiza,
kama safarini kuna milima na mabonde,
ni kama shida zitakazo kupiga makonde,
unone ama ukonde,
siwezi hubiri yale hayako,
video zangu ni za kifahari ilihali mie sina makao,
hii mistari na kwa wasanii,
tuwe kama mwangaza kwa jamii,
mafanikisho ni kama mabadiliko yataishi milele,
angaza kama nyota ukifika kwenya killele,
kila mtu atambue kuna nuru mlimani..

Kwisha


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

They Rule The Streets

Classic Poetic Love

Business Plan Competition